You are currently viewing DADDY ANDRE ATAKA WAANDISHI WA NYIMBO NA MAPRODYUZA KUPEWA KIPAU MBELE UGANDA

DADDY ANDRE ATAKA WAANDISHI WA NYIMBO NA MAPRODYUZA KUPEWA KIPAU MBELE UGANDA

Msanii na Prodyuza Daddy Andre amedai kwamba maprodyuza na waandishi wa nyimbo wanachukuliwa poa nchini uganda licha ya wao kuwa nguzo muhimu kwenye tasnia ya muziki.

Katika mahojiano yake hivi karibuni Daddy Andre amekiri kutofaidi na kipaji chake cha uandishi wa nyimbo huku akipendekeza wasanii waanze kugawana na waandishi wa nyimbo asilimia 50 ya mapato ya nyimbo zao.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Kola” amesema uandishi wa nyimbo inahitaji ubunifu na muda mwingi ila mwisho wa siku waandishi wa nyimbo huambulia patupu jambo ambalo amedai sio cha kingwana.

Hata hivyo ametoa wito kwa wabunge kutunga sheria itakayowalinda waandishi wa nyimbo na maprodyuza ila waanze kupata mgao wa mapato wa nyimbo wanazozifanyia kazi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke