Msanii na Prodyuza kutoka Uganda Daddy Andre ametoa onyo kwa Nina Roz kukoma kutumia nyimbo alizomuandikia kipindi wanafanya kazi pamoja kwenye shows zake.
Kupitia barua ya mawikili wake Daddy Andre amemtaka Nina Roz amlipe shillingi millioni 120 za Uganda la sivyo atamfungulia kesi mahakamani.
Kulingana vyanzo vya karibu na Daddy Andre, prodyuza huyo anataka alipwe shillingi millioni 30 za Uganda kwa kila wimbo aliomuandikia Nina Roz.
Nyimbo hizo ni kama Nangana, Billboard Kipande, Enyonta, na Andelle.
Wawili hao walisaini mkataba wa kufanya kazi pamoja mwaka wa 2020 lakini walikuja wakaachana mwaka wa 2021 baada ya kuingia ugomvi na tangu wakati huo wamekuwa wakirushiana maneno makali kwenye mahojiano mbali mbali.
Notisi hiyo ya Daddy Andre inakuja wakati huu Nina Roz amefungua kesi polisi akimtuhumu prodyuza huyo kumuibia gari aina Mark X.
Inadaiwa Daddy Andre alichukua gari la Mrembo huyo kama malipo ya kazi ambayo prodyuza huyo alimfanyia kipindi wanafanya kazi pamoja.