Msanii na Prodyuza kutoka nchini Uganda Daddy Andre ametuhumiwa kumuibia gari mpenzi wake wa zamani Nina Roz.
Kulingana na kesi iliyowasilishwa kwa polisi Daddy Andre alimuomba Nina Roz gari atumie kwenye shughuli zake mwaka wa 2020 lakini alikataa kumrudisha gari hilo.
Kwenye taarifa ya polisi, Nina Roz anadaiwa kununua gari hilo kwa mkopo mwaka 2020 ambapo alilipa shillingi millioni 10 za uganda kati ya shillingi millioni 21 alizokuwa anadaiwa.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Daddy Andre ambaye alikuwa shahidi wa Nina Roz wakati ananunua gari hilo alibadilisha umiliki wa gari na kuwa lake baada ya mpenzi wake huyo wa zamani kumpokeza shillingi millioni 11 za uganda akamilishe deni la gari hilo.
Hata hivyo dalali aliyebadilisha usijali wa gari kutoka kwa Nina Roz kwenda Daddy Andre tayari ametiwa mbaroni huku polisi wakiendelea na uchunguzi kubaini ukweli kuhusu sakata hilo.