You are currently viewing Daddy Owen aahirisha hafla yake ya kila mwaka ya Malaika Disability Walk.

Daddy Owen aahirisha hafla yake ya kila mwaka ya Malaika Disability Walk.

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Daddy Owen ameahirisha hafla yake ya kila mwaka ya Malaika Disability walk ambayo ilipangwa kufanyika tarehe 3 Desemba mwaka huu.

Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Owen alisema matembezi hayo hayatafanyika kutokana na kifo cha kusikitisha cha binamu yake Stephen Sunrise Osedo ambaye atazikwa siku hiyo, hivyo wamelazimika kusogeza mbele hadi Machi 4 mwaka 2023.

“Kutokana na mazingira yasiyoepukika, tulilazimika kuahirisha MATEMBEZI YA WALEMAVU YA MALAIKA 2022 ambayo yalipangwa kufanyika tarehe 3 Desemba ambayo ni SIKU YA WALEMAVU DUNIANI! Mazishi yatakuwa tarehe hiyo hiyo (tarehe 3 Desemba)”

“”Wakati huo huo shule nyingi za Msingi zimeomba ushiriki wa MATEMBEZI, hivyo tumebadilisha tarehe kuwa MACHI 4, 2023. Tunaomba msaada wenu kikamilifu na tunaomba radhi kwa wadau wote waliokuwa wamejitokeza kutuunga mkono.#MalaikaDisabilityWalk2023.”, Aliandika.

Binamu yake Owen aliuawa kwa kupigwa risasi na afisa wa polisi huko Umoja, kaunti ya Nairobi wiki mbili zilizopita.

Daddy Owen alianzisha hafla ya Malaika mwaka 2012 kwa lengo la kutambua mchango wa watu wenye changamoto ya ulemavu katika jamii.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke