You are currently viewing DADDY OWEN AICHARUKIA JARIDA MOJA KWA KUCHAPISHA TAARIFA ZA UONGO KUHUSU UTAJIRI WAKE

DADDY OWEN AICHARUKIA JARIDA MOJA KWA KUCHAPISHA TAARIFA ZA UONGO KUHUSU UTAJIRI WAKE

Msanii wa nyimbo za injili Daddy Owen ameibuka na kukanusha taarifa za utajiri wake zilizoainishwa na jarida moja kuwa ana utajiri wa shilllingi millioni 938 za Kenya.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema kuna watu walimfanyia mahojiano kwa njia ya  simu na walipomuuliza swali la utajiri alisusia lakini cha kushangaza alitumiwa taarifa kuwa ana utajiri dollar million 8 jambo ambalo amedai kuwa data hizo ni batili.

“Someone called me for a phone interview, in the middle of the interview they asked me, how much are u worth? I said “pass” .. After a few minutes they sent me ths.. “, Ameandika Instagram.

Msanii huyo amesema jarida hilo lilipaswa kufanya uchunguzi kwanza kabla ya kumuweka kwenye orodha ya mastaa ambao wana mkwanja mrefu.

“Ngoja kwanza, before utoe calculator uanze kupiga hesabu ya $8M ni how much in Kshs. Mimi niko na swali tu moja, hawa watu walijuaje?? Nani aliwaambia?? Sasa nafaa “Amen” or “uongo”🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔😳😳😳😳😳😳😳 n btw.. I have just landed from Harare.. #ifyouknowyouknow😉”, Amekazia.

Hii sio mara ya kwanza kwa mastaa kuwekewa utajiri usio wao, mapema mwaka jana Jarida la Forbes lilimweka Diamond Platnumz kwenye orodha ya wanamuziki tajiri Barani Afrika jambo ambalo lilimfanya msanii huyo kuijua juu jarida hilo kwa kuchapisha taarifa za uongo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke