Mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini Daddy Owen amekanusha madai ya kutoka kimapenzi na rafiki wake wa karibu Eve Maina.
Kupitia instastory yake amesema hana uhusiano wowote wa kimapenzi na mrembo huyo huku akisema ukaribu wao ni wa kirafiki.
Msanii huyo ambaye kipindi cha nyuma alitangaza kuwa anatafuta mke,amesema hatokuja kuweka wazi mahusiano yake kwa umma mtandaoni.
“Hapo sijui, but ata kama nitaoa tena I would wish for something very very private,”Aliandika
Kauli ya Daddy Owen inakuja mara baada ya shabiki kumuuliza kama anachumbiana na mrembo huyo.