You are currently viewing DADDY OWEN AKANUSHA TETESI ZA KUTOKA KIMAPENZI NA BRENDA WAIRIMU

DADDY OWEN AKANUSHA TETESI ZA KUTOKA KIMAPENZI NA BRENDA WAIRIMU

Staa wa muziki nchini Daddy Owen amevunja kimya chake juu ya tuhuma za kumtaka kimapenzi mwiigizaji Brenda Wairimu kupitia mitandao yake ya kijamiii.

Kupitia ukurasa wake wa instagram Daddy Owen ameonyesha kufurahishwa na namna watu walifsiri ujumbe wake kwenda kwa brenda wairimu huku akisema kwamba hana uhusiano wowote wa kimapenzi na mrembo huyo.

Hitmaker “Vanity” ameenda mbali zaidi na kuahidi kumpeleka Brenda Wairimu kwenye mtoko mbele ya wanablogu ili kuzima tetesi za kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwiigizaji huyo, jambo ambalo lilimfanya mrembo huyo kushuka kwenye uwanja wa comment ya post ya Daddy Owen na kukubali ombi lake.

Kauli ya Daddy Owen imekuja mara baada ya kuachia ujumbe kwenye picha ya Brenda Wairimu, ujumbe ambao uliibua maswali mengi miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii ambao walihoji kwamba huenda wawili hao wanatoka kimapenzi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke