You are currently viewing DADDY OWEN AWABARIKI MASHABIKI ZAKE NA CHAPTER 4 ALBUM

DADDY OWEN AWABARIKI MASHABIKI ZAKE NA CHAPTER 4 ALBUM

Mwanamuziki wa nyimbo za Injili nchini Daddy Owen ameachia rasmi album yake mpya iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki zake.

Album hiyo inayokwenda kwa jina la Chapter 4 ina jumla ya singo 15 ya moto huku ikiwa na 6 collabo pekee.

Daddy Owen amewashirikisha wasanii kama Nakaaya,Bella Kombo, Judy Stevens,Ivyln Mutua,Danco na Slejj.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa chapter 4 album  Daddy Owen amesema safari ya kuandaa album yake mpya haikuwa rahisi ila anamshukuru mwenyezi mungu kwa kumwezesha kuikamilisha album hiyo licha ya changamoto alizokutana nazo.

Chapter 4 ni album ya sita kwa mtu mzima Daddy Owen lakini pia inavunja ukimya wake wa miaka 5 tangu alipoachia album yake ya Vanity iliyotoka mwaka wa 2016.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke