Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Daddy Owen amewashauri mastaa kurudisha mkono kwa jamii kwa kutoa misaada kwa watu wenye uhitaji.
Kupitia instagram Daddy Owen amesema hatua hiyo itawapa motisha wakenya kuwasaidia wakati matatizo badala ya kuisha maisha ya kuigiza kwenye mitandao ya kijamii.
Hitmaker huyo wa Yahweh amesema kipindi alijipata kwenye matatizo hakuna staa hata mmoja alijitokeza kumsaidia ila anamshukuru mungu mashabiki zake ndio walikuwa mstari wa mbele kumshika mkono hadi akarudi katika hali yake ya kawaida.
Daddy Owen ametoa kauli hiyo akijibu swali la mchekeshaji Creative Terrence ambaye alitaka kufahamu ni kitu gani inawafanya wakenya kutowasaidii mastaa mbali mbali nchini wakati wana changamoto katika maisha.
Swali la Terrence liliibua hisia mseto miongoni mwa wakenya mtandaoni ambao wamehoji kuwa wasanii wanaishi maisha ya kifahari kwenye mitandao ya kijamii jambo limewafanya wengi wake kutoamini kama kweli huwa wanapata maishani.