Mwanamuziki David Lutalo amejiunga na orodha ya waimbaji wanaomuunga mkono King Saha kutua wadhfa wa urais wa Chama cha Wanamuziki wa Uganda (UMA).
Katika mahojiano yake ya hivi karibuni David Lutalo amesema kwa miaka ambayo amemfahamu King Saha, alikuja akagundua kuwa msanii huyo ni mtu mwerevu tofauti namna watu wanavyochukulia.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Mboona” amepuuzilia mbali madai ya watu wanaodai kuwa King Saha hawezi waongoza wasanii nchini Uganda kutokana na kuathirika na matumizi ya mihadarati.
“Nasikia watu wakisema kwamba anavuta bangi, lakini nadhani gugu lake haliendi kichwani. Ni mtu mwenye mawazo mazuri unapotangamana naye,” Lutalo alisema.
Lakini pia ameongeza kuwa King Saha ni mweelewa na anaweza fanya kazi vizuri na hata watu walio chini yake.
Hata hivyo alitaka kuwania wadhfa wa urais wa muungano wa wanamuziki nchini uganda lakini alikuja akajiondoa katika kinyanganyiro hicho kutokana na kukosa vigezo stahiki.
Utakumbuka David Lutalo anajulikana kuwa mtu asiyeweza kufikiwa kwa urahisi tangu umaarufu ulipomuingia kichwani mwake