Msanii wa nyimbo za injili nchini David Wonder amefunguka kuhusu ukimya wake kwenye muziki.
Akipiga stori na mpasho David Wonder amesema kwamba aliamua kuacha kila kitu na kujifirikia kwanza kama njia ya kujitibu baada ya kukumbwa na tatizo la afya ya akili.
Aidha ameenda mbali zaidi na kukiri kutopata chochote kwenye muziki wake ikiwemo kutomiliki hadi kazi zake za muziki ambazo amezifanya kwa kipindi chote ambacho alikuwa chini ya lebo ya muziki ya EMB Records inayomilikiwa na Bahati.
Hata hivyo hitmaker huyo “Ndogo Ndogo” amedokeza mpango wa kuanza kuifanyika kazi album yake mpya mbayo kwa mujibu wake itaingia sokoni mwakani.