You are currently viewing DAVID WONDER ANYOSHA MAELEZO KUHUSU BIFU LAKE NA BAHATI

DAVID WONDER ANYOSHA MAELEZO KUHUSU BIFU LAKE NA BAHATI

Msanii wa nyimbo za injili nchini David Wonder amefunguka kuhusu ishu ya kuwa kwenye bifu na staa wa muziki nchini Bahati mara baada ya nyimbo zake alizofanya na msanii huyo akiwa chini ya lebo ya EMB kufutwa kwenye mtandao wa Youtube.

Akipiga stori na mwanahabari Nicholas Kioko kwenye mtandao wa Youtube David Wonder amesema hana ugomvi wowote na msanii huyo licha ya kwamba amekuwa akimzungumzia vibaya kwenye mahojiano mbali mbali.

Hitmaker huyo wa “Naenda na Yesu” amekanusha ishu ya kupotea kimuziki kwa kusema kwamba amekuwa akiachia ngoma bila kupoa ila vyombo vya habari nchini Kenya vimekuwa vikiwangazia wasanii ambao wamekuwa na drama nyingi kwenye tasnia ya muziki huku wasanii wanaotoa muziki mzuri wakisahulika

Hata hivyo amedokeza kuachia album yake mwaka huu wa 2022 huku akiwataka mashabiki zake kukaa mkao wa kula kupokea ujio wake mpya ambao ameutaja kama  wakitofauti zaidi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke