Mwanamuziki wa nyimbo za injiili Nchini David Wonder ametusanua kuwa album yake mpya iitwayo mwanzo imekamilika.
Wonder amesema album yake itaingia sokoni rasmi Desemba 10 mwaka huu huku akiwa amewashirikisha wasanii mbali mbali wa nyimbo za injili kutoka Afrika Mashariki.
Licha ya kutoweka wazi idadi ya nyimbo inayopatikana kwenye mwanzo album, David Wonder amewataka mashabiki wakae mkao wa kula kuipokea Album yake hiyo.
Hii itakuwa ni album ya kwanza kwa mtu David Wonder tangu aanze safari yake muziki.