Staa kutoka Nigeria Davido amefanikiwa kufikisha jumla ya wafuatiliaji (Subscribers) Milioni 3 katika channel yake ya youtube.
Davido anakuwa msanii wa pili kwa nchini Nigeria kuwa na subscribers wengi katika mtandao wa youtube.
Nafasi ya kwanza inashikwa na mwimbaji nyota CKay mwenye subscribers Milioni 3.16 akiwaacha mbali Burna Boy mwenye subscribers million 2.54 huku Wizkid akiwa na Subscribers million 2.41.