You are currently viewing Davido ahairisha tamasha lake la muziki nchini Marekani

Davido ahairisha tamasha lake la muziki nchini Marekani

Mwanamuziki wa Nigeria Davido hatafanya tena tamasha lake “AWAY” la nchini Marekani ambalo lilikuwa likisubiriwa kwa hamu, hii ni kufuatia kifo cha mwanaye ambaye alifariki dunia wiki iliyopita.

Menejimenti ya Davido imetoa taarifa rasmi kwamba Tamasha la msanii huyo ambalo lilikuwa lifanyike Novemba 18 mwaka huu katika uwanja wa State Farm Arena Jijini Atlanta Georgia, limeahirishwa hadi Novemba 18, mwaka 2023

Menejimenti yake imesema ni muhimu kwa Davido kutumia muda huu na familia yake pamoja na wapendwa wake. Kwa wote waliokuwa tayari wamenunua tiketi, basi zitatumika mwakani siku ya onesho hilo. Bado Davido na Chioma hawajazungumza chochote tangu tukio la kumpoteza mtoto wao

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke