You are currently viewing DAVIDO AJIZAWADIA LAMBORGHINI

DAVIDO AJIZAWADIA LAMBORGHINI

Davido ameongeza gari lingine kwenye orodha ya magari yake ya kifahari, leo mwimbaji huyo amejizawadia gari aina ya Lamborghini Aventador ambapo inatajwa kuwa ametoa kiasi cha ($550k) zaidi ya shillingi millioni 62.1 kuinunua.

Kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram amebainisha kuwa hatonunua tena gari lingine kwa muda kidogo baada ya kuvuta ndinga hilo.

Hii ni gari ya pili ya kifahari kuingia kwenye mikono ya Davido ndani ya miezi 6, mwezi Mei mwaka huu alinunua gari aina ya Rolls Royce Cullinan yenye thamani ya ($500k) zaidi ya shillingi millioni 56.5, hivyo ametumia zaidi ya shillingi millioni 112.8 kununua magari mawili ndani ya miezi 6.

Ikumbukwe wiki chache tu zimepita tangu akusanye zaidi ya millioni 49 za Kenya za kutoka kwa wasanii pamoja na watu wake wa karibu, ambao walimchangia kwa ajili ya birthday yake, lakini aliamua kupeleka pesa hizo katika vituo vya watoto ya yatima nchini kwao Nigeria.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke