Staa wa muziki kutoka Nigeria Davido ameendelea kuchana mbuga Kimataifa mara baada ya kutokea kwenye cover la jarida maarufu la burudani nchini Uingereza.
Kupitia toleo hili jipya la Jarida hilo, limeangaza maisha ya Davido kwa undani na jinsi alivyofanikiwa na namna alivyoweza kusapoti vipaji vingine nchini humo pasipo kuingiza biashara ndani yake.
“Lebo yangu sio biashara, ninatoa fursa kwa sababu kuna watu wengi wenye vipaji nchini Nigeria” amesema Davido akiliambia jarida la Wave Magazine.
Mbali na hilo pia amezungumzia juu ya kuendelea kupanua ushawishi wa Kimataifa katika muziki wa Afrobeats.