You are currently viewing DAVIDO AKERWA NA MAPROMOTA WA MUZIKI NCHINI ITALIA

DAVIDO AKERWA NA MAPROMOTA WA MUZIKI NCHINI ITALIA

Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria Davido ameeleza masikitiko yake kufuatia kutolipwa pesa zake na waandaaji wa tamasha la muziki nchini Italia

Kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram, kwa uchungu Davido amesema wasanii wanapitia magumu ya kuchosha miili yao kwa jasho na machozi, yote kwa ajili ya mashabiki zao lakini wanaishia kuchukuliwa poa na mapromota.

Davido amefunguka kwamba alifika kwenye show hiyo nchini Italia kwa safari ya ndege tatu za kuunganisha, mwisho wa siku promota anashindwa kumlipa pesa zake hadi dakika ya mwisho, licha ya kuuza tiketi takribani Elfu 7.

Kwa heshima ya mashabiki zake ambao wamelipa pesa kwa ajili ya kumuona, Davido amesema aliamua kupanda stejini na kufanya show hiyo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke