You are currently viewing DAVIDO ALAMBA DILI NONO LA KUWA BALOZI WA KAMPUNI YA PUMA

DAVIDO ALAMBA DILI NONO LA KUWA BALOZI WA KAMPUNI YA PUMA

Davido ametangaza kusaini dili nono la kuwa balozi wa kampuni maarufu ya mavazi ya michezo duniani PUMA.

Mkali huyo kutoka nchini Nigeria atakuwa na jukumu la kuitangaza kampuni hiyo kwenye soko la Afrika ambalo linakuwa kwa kasi.

Kwa mujibu wa ripoti, inaelezwa kuwa Davido pia atakuwa na jukumu la kuitangaza PUMA kwenye eneo la kusini mwa jangwa la Sahara, Amerika ya Kaskazini na dunia kwa ujumla.

Davido atakuwa akivaa mavazi ya kampuni hiyo kama miongoni mwa makubaliano yao na pia kufanya matangazo ya michezo kama mpira wa Kikapu na mpira wa Miguu.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke