Mwanamuziki nyota wa Nigeria Davido ametumia zaidi ya shilingi million 689 za Kenya kununua kiwanja katika eneo la kifahari nchini Nigeria, Banana Island.
Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram Davido amesema amenunua eneo hilo kwa ajili ya kujenga nyumba ya ndoto yake.
Davido ambaye ni mkazi wa eneo hilo, anaongeza idadi ya nyumba nyingine Banana Island kwani tayari anamiliki Jumba la kifahari ambalo alilinunua mwaka 2020 kwa zaidi ya shilling million 157 za Kenya.