Kwa kawaida, kwenye kila sherehe au matatizo, suala la michango huwa ni kigugumizi kikubwa kwa watu wengi Duniani
Hii imekua tofauti kidogo kwa staa wa muziki kutoka nchini Nigeria Davido Ambaye amekuja na mbinu tofauti ya kupata zawadi kutoka kwa marafiki zake kwenye siku ya Kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.
Goodnews ni kwamba Davido tayari amepokea kiasi cha (Naira 181M) zaidi ya shillingi millioni 49 kutoka kwa marafiki zake wa karibu pia mashabiki wa muziki ikiwa ni siku mbili tangu atangaze kuomba achangiwe pesa kwa ajili ya kusheherekea siku yake ya kuzaliwa, Novemba 21 mwaka huu.
Sasa huenda Davido asizitumie kabisa pesa hizo kama ambavyo alikuwa amepanga, kupitia ukurasa wake wa Twitter ametangaza kuwa anaweza kuzigawa kwa wenye uhitaji.