You are currently viewing DAVIDO KUGAWA MTAJI WA SHILLINGI MILIONI 5.5 KWA WATU 20 NIGERIA

DAVIDO KUGAWA MTAJI WA SHILLINGI MILIONI 5.5 KWA WATU 20 NIGERIA

Staa wa muziki kutoka nchini Nigeria Davido ametangaza habari njema kwa raia nchini humo kuwa ana mpango wa kugawa shillingi Milioni 5 za Kenya kwa watu 20  walio na mawazo ya biashara ili wajikwamue kiuchumi.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Davido ameeleza kwamba anahisi serikali ya Nigeria imeshindwa kusaidia raia wake kukua kiuchumi kwani raia wengi kwa sasa wanategemeana kuinuana kimaisha.

Hata hivyo, amewataka raia wa Nigeria kumtumia mawazo ya kibiashara na atachagua washindi ambao atawapa kiasi hicho cha pesa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka blogu mbalimbali za Nigeria ni kwamba tayari watu wengi wametoa mawazo yao ya kibiashara kwa mwanamuziki huyo na wanasubiri kuona ikiwa watabahatika.

Mpango wa kugawa shilling Milioni 5 za Kenya kwa watu 20 umepangwa kufanyika leo Machi 18.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke