Nyota wa muziki kutoka nchini Nigeria davido ametangaza kufanya show kwenye ukumbi maarufu wa burudani duniani 02 Arena uliopo nchini Uingereza.
Davido ametoa tangazo hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ameweka wazi kuwa March 5,mwaka wa 2022 ndio tarehe rasmi ambayo watu takribani Elfu 20 watashuhudia show yake nchini Uingereza.
Hii si mara ya kwanza kwa mtu mzima Davido kutumbuiza kwenye ukumbi huu mkubwa wa burudani kwani mnamo Januari 28, mwaka wa 2019 aliujaza ukumbi huo na kushusha mvua ya burudani