You are currently viewing Davido mbioni kufunga ndoa mwaka 2023

Davido mbioni kufunga ndoa mwaka 2023

Staa wa muziki kutoka nchini Nigeria Davido ameahidi kuwa mwaka 2023 atafunga ndoa na mpenzi wake Chioma.

Davido amebainisha hayo akiwa na baby mama wake huyo pamoja na mchungaji wake Tobi Adegboyega huko Uingereza, alipoenda kumtambulisha Chioma kwa mchungaji huyo.

“Our wife, our real wife,” anasikika Mchungaji Tobi akieleza, na Davido akaongezea, “Hundred per cent, going down 2023.”

Mbali na hilo kupitia instastory ya Staa davido ameshare picha na video zikionesha mpenzi wake Chioma akipewa zawadi ya Mkoba na Mchungaji tobiadegboyega_Ambapo mkoba huo unatajwa kuwa na Thamani ya $90,000 zaidi ya million 9 za Kenya.

Ikumbukwe, Davido na Chioma walianza mahusiano yao tangu mwaka 2017, na 2019 Davido alimvisha pete ya uchumba Chioma. Hata hivyo wakaja kuachana mwaka 2020, wakabaki kuwa walezi wa mtoto wao. Julai mwaka huu wakawa wanahusishwa kurudiana, kisha baadae wakathibitisha na sasa wamepanga kufunga pingu za maisha ifikapo mwakani.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke