Mwanamuziki nyota kutoka nchini Nigeria Davido amethibitisha uwepo wa collabo yake na rapa kutoka nchini Canada Drake mwaka wa 2022.
Kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram Davido ameshare sehemu ya video akiwa anazungumza na rapa huyo kupitia video call na kusindikiza na ujumbe unao ashiria uwepo wa collabo kati yao ifikapo mwaka wa 2022.
Kama collabo hiyo itafanikiwa basi Davido atakuwa msanii wa pili mkubwa kutoka Nigeria kufanya kazi na Drake ikizingatiwa kuwa kipindi cha nyuma alifanya kazi ya pamoja na WizKid kupitia nyimbo kama ‘Closer & One dance’