Staa wa muziki kutoka Nigeria Davido ameripotiwa kufunga ndoa na mpenzi wake Chioma ambaye ni mzazi mwenza wa mtoto wao aliyefariki dunia “Ifeanyi”. Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari toka Nigeria.
Ndoa hiyo inayotajwa kuwa ya kitamaduni ilifungwa nyumbani kwa baba yake Davido na ilihudhuriwa na watu wa familia za wawili hao pekee. Katika hafla hiyo, inaelezwa hakuna aliyekubaliwa kupiga picha wala kuchukua video.
Pia inaelezwa, mahari ya Chioma ililipwa yote ingawaje alikuwa amekataa kuolewa na Davido kufuatia kifo cha mwanae ambaye alimtizamia kama ndiye aliyewaleta pamoja.
Ndoa hiyo ilikuwa sharti ifungwe ili Ifeanyi ambaye alifariki kwenye swimming pool nyumbani kwao, aweze kuzikwa kama mmoja wa familia ya Davido, kulingana na tamaduni za jamii ya Igbo.
Aidha, kabla ya kifo cha Ifeanyi, Davido na Chioma walikuwa tayari wametangaza rasmi kwamba watafunga ndoa mwakani 2023.