You are currently viewing DAVIDO NA DJ MAPHORISA WARUSHIANA MANENO MAKALI MTANDAONI KISA AMAPIANO

DAVIDO NA DJ MAPHORISA WARUSHIANA MANENO MAKALI MTANDAONI KISA AMAPIANO

Staa wa muziki kutoka Nigeria Davido amemjibu DJ Maphorisa kufuatia mjadala uliozuka kwenye mtandao wa twitter juu ya msanii aliyeutangaza zaidi muziki wa Amapiano kimataifa.

Kupitia moja ya watumiaji wa twitter alishare ujumbe kuwa msanii Davido ndio msanii aliyeutangaza muziki wa Amapiano Afrika na kimataifa na kudai kuwa kwa sasa msanii Wizkid ndio anajaribu kufanya kama alivyofanya Davido huku akidai kuwa msanii huyo amekuwa akianza kufanya vitu na wasanii wengine wanaiga kwake.

Baada ya ujumbe huo mkali kutoka nchini Afrika Kusini DJ Maphorisa aliijibu tweet hiyo na kusema kuwa yeye na Kabelo Motha walianza kuwashirikisha wasanii Wizkid na Burna Boy kwenye wimbo wa Amapiano wa Sponono miaka mitatu nyuma, hivyo sio Davido aliyeutangaza muziki huo.

Kauli hiyo imemuibua Davido ambaye ameshindwa kukaa kimya kuhusu mjadala huo na kuandika kuwa DJ Maphorisa hajawahi kumpenda licha ya kuwa mtu mwema kwake, hivyo ameamua kujiweka mbali naye.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke