You are currently viewing DAVIDO NA KIZZ DANIEL MBIONI KUACHIA EP YA PAMOJA

DAVIDO NA KIZZ DANIEL MBIONI KUACHIA EP YA PAMOJA

Mastaa kutoka Nigeria Davido na Kizz Daniel wamewadokezea mashabiki wa muziki wao juu ya ujio wa EP ya pamoja.

Kupitia twitter wamethibitisha taarifa hiyo huku Davido akitamba kwamba EP hiyo itauza nakala milioni kwenye wiki ya kwanza.

“Nani yuko tayari kwa ajili ya Ep ya 0.B.O X KIZZ?? Tutauza zaidi ya Milioni 1 katika wiki ya kwanza tu” ametweet Davido.

Hata hivyo wawili hao hawajaweka wazi tarehe rasmi ya kuachia EP hiyo wala jina lake.

Mara ya mwisho Wakali hao kukutana ilikuwa kwenye singo iitwayo “One Ticket” kutoka kwenye Album ya Kizz Daniel “No Bad Songz” ya mwaka 2018.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke