Wanamuziki wa Nigeria Davido na WizKid ni kama wamemaliza tofauti zao ,mara baada ya kukutana kwenye moja ya club huko jijini Lagos nigeria na kukumbatiana huku wakionekana kuwa na furaha kila mmoja.
Wanamuziki hao mara kadhaa wametajwa kuwa kwenye ugomvi, na katika hili wanaongeza idadi ya wanamuziki waliopatana ndani ya mwaka huu baada ya Burna Boy kutangaza kumaliza tofauti zake na Davido.
Hata hivyo mashabiki wa muziki nchini Nigeria wameonekana kufurahia hatua ya Davido na Wizkid kumaliza ugomvi wao huku wakiwataka wawili hao kuachia ngoma ya pamoja.