Tume ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini Nigeria (ICPC) imemkamata Mwanamuziki Oladapo Oyebanji almaarufu kama D’Banj kwa madai ya utapeli wa kuchepusha mamilioni ya pesa za mradi wa N-Power.
Vyombo vya habari nchini Nigeria vinaripoti kwamba D’Banj amefanya utapeli huo kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa serikali. Mradi wa N-Power ulianzishwa mwaka 2016 na Rais Muhammadu Buhari ambapo lengo kuu ni kusaidia vijana wasio na ajira kwa kuwapatia pesa.