Msanii wa muziki nchini Dogo Richie amedai kuwa waandaaji wa matamasha ya muziki nchini Kenya wamekuwa na tabia ya kuwa dhulumu wasanii kutokana na wao kukosa elimu kuhusu mikataba
Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Dogo Richie amesema wandaaji wengine wa tamasha wamekuwa wakiwabadilishia malipo wasanii baada ya kutumbiza kwenye tamasha kwa kutoa sababu zisizo kuwa na msingi wowote.
Lakini pia amewalaumu baadhi ya wasaani ambao amesema wamekuwa na hulka ya kuingia mikataba na mapromoter hao kwa njia ya kishikaji, jambo ambalo limepelekea wanamuziki wengi nchini kudharauliwa kwenye shows.
Hata hiyo Dogo Richie ambaye kwa sasa anafanya poa na ngoma yake iitwayo “Hae” amesema atahakikisha kuwa makubaliano yote kati yake na promoter yeyote yana nakiliwa kama njia ya kuepuka kutapeliwa.