You are currently viewing DENNO MUSIC AZINDUA MPANGO WA 47 FOR PEACE UNAOLENGA KUHUBIRI AMANI MIONGONI MWA VIJANA

DENNO MUSIC AZINDUA MPANGO WA 47 FOR PEACE UNAOLENGA KUHUBIRI AMANI MIONGONI MWA VIJANA

Msanii wa nyimbo za injili nchini Denno amezindua mpango wa 47 For Peace kwa ushirikiano na shirika la Jitwak ambao unalenga  kuhubiri amani miongoni mwa vijana kabla na hata baada ya uchaguzi wa mwaka wa 2022.

Akizungumza kwenye mkao na wanahabari Denno amesema wanapania kuzuru kaunti  zote 47 za humu nchini kwa ajili kutoa elimu kwa vijana kuhusu umuhimu wa kudumisha amani wakati taifa linapoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa 2022 kwani mara nyingi vijana hutumiwa na wanasiasa  kuzua vurugu wakati kampeini  za kisiasa.

wa upande wake mwenyekiti  wa shirika la Jitwak George Ochieng amesema wananuia pia kuwashirikisha wasanii wengine kufanikisha mpango wa 47 for peace huku akitoa wito kwa wananchi na serikali za Kaunti kuwaunga mkono katika juhudi zao za kuhubiri amani mwiongoni mwa vijana.

Kampeini ya kuhubiri amani na utangamano ya 47 for Peace itaanza ziara yake ya katika kaunti ya Nairobi na Kiambu mtawalia kabla ya kuzuru maeneo mengine ya nchi kenya.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke