Msanii kutoka uganda Desire Luzinda, ametangaza kurejea muziki baada ya kukaa kimya kwa takriban miaka minne.
Kupitia mitandao yake ya kijamii Desire Luzinda amethibitisha kuachia wimbo mpya wa Injili kutoka kwenye EP yake mpya “ALABASTER HEART” ambayo amekuwa akiifanyia kazi.
“Mabibi na mabwana, kila kitu kina msimu na wakati wake. Baada ya miaka minne ya ukimya, ninafurahi kutangaza kwamba nitatoa wimbo wangu wa kwanza kutoka kwenye EP yangu ya ALABASTER HEART EP Hivi karibuni. Nimefurahia sana kile ambacho Bwana anakaribia kufanya,” aliandika.
Luzinda hajakuwa akiachia nyimbo tangu alipoacha muziki wa kidunia mwaka wa 2019 na kugeukia muziki wa injili.
Kwa sasa anaishi nchini Marekani lakini amekuwa akifanya kazi kwa ukaribu na watayarishaji na wasanii wa Uganda hasa Levixone ambaye alimsaidia kwenye project yake mpya.