You are currently viewing DIAMOND AFUNGUKA CHANZO CHA KUTOSHIRIKI TUZO ZA TANZANIA MUSIC AWARDS

DIAMOND AFUNGUKA CHANZO CHA KUTOSHIRIKI TUZO ZA TANZANIA MUSIC AWARDS

Staa wa Muziki wa Bongofleva Diamond Platnumz amefunguka sababu zilizomfanya asishiriki Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) zilizomalika majuzi.

Akizungumza na BBC Swahili jijini London, Uingereza, anasema kuwa kikubwa kilichomfanya asishiriki Tuzo hizo ni imani maana mara ya kwanza alinyimwa Tuzo wakati alistahili kupata na yeye ndo sababu ya Tuzo Kusitishwa kwa zaidi ya Miaka 9.

Mbali na hayo, amekunusha madai kuwa mama yake mzazi, Bi. Sandra maarufu kama Mama Dangote ndiye amekuwa akimpangia mwanamke wa kumuoa.  Diamond amesema kwa sasa yeye ni mtu mzima hawezi kupangiwa na wanaozusha hilo wanamkosea sana mama yake.

“Hapana kwanza wanamkosea sana mama yangu, hawezi kunipangia kwa umri wangu niliofika kweli nitapangiwa na mzazi?, hayo maisha yameshaishia zamani sana kwa kupangiwa na mzazi umuoe nani, usimuoe nani, mama yangu hawezi kunipangia,” amesema Diamond.

Hata hivyo  amefunguka matamanio yake ya kuukimbia ubachela na kuingia kwenye maisha ya ndoa kwa kusema, “Kila binadamu anataka kuoa, nitaoa, natamani kuoa, naelekea kuoa, hiyo ni kauli sahihi zaidi, Bibi harusi watu watamuona. Natamani nitulie. Ubaya wa Watanzania wanataka kumpangia mtu muda wake, pengine bado sijajitosheleza kimaisha,”

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke