Baada ya kuweka kambi nchini Marekani kwa takribani wiki tatu, hatimaye staa wa Muziki wa bongofleva diamond platnumz amehitimisha ziara yake nchini humo.
Diamond alianza ziara yake Jijini Atlanta mnamo October 8, mwaka wa 2021 na kuhitimisha Dallas mnamo October 31, mwaka 2021.
Baada ya kumalizana marekani Diamond anatarajia kuanza tour yake barani Ulaya.
Hii ni kwa mujibu wa meneja wake sallam sk ambaye ameandika kupitia ukurasa wake wa instagram ujumbe unaosomeka “Tumemaliza ziara ya Marekani, asanteni wote. Kaeni tayari kwa ziara ya Ulaya”