You are currently viewing DIAMOND AINGIA STUDIO NA MOHAMMED RAMADAN KUANDAA WIMBO WA PAMOJA

DIAMOND AINGIA STUDIO NA MOHAMMED RAMADAN KUANDAA WIMBO WA PAMOJA

Mwanamuzi kutoka Tanzania,Diamond Platnumz ameingia studio kurekodi wimbo na staa wa muziki kutoka nchini Misri, Mohamed Ramadan.

Diamond ameingia studio na staa huyo ambaye ni mbabe wa youtube afrika kwa upande wa wasanii kwani anazaidi ya subscribers zaidi ya milioni 13.3 kwenye mtandao huo huku akiwa amevuna jumla ya watazamaji zaidi ya bilioni 4.3 kwenye mtandao huo wa youtube.

Diamond na Mohamed wamekutana jijini Dubai ambapo wote walikuwa wamealikwa kwenye tamasha la All Africa Festival lililofanyika usiku wa kuamkia October 22,mwaka wa 2021.

Ikumbukwe Diamond Platnumz ndiye alikuwa msanii wa kwanza Afrika Mashariki na kati kufikisha jumla ya watazamaji bilioni 1 kwenye mtandao wa youtube lakini pia ndiye msanii mwenye subscribers wengi kwa wasanii wa wanaopatikana kusini mwa Jangwa la Sahara.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke