You are currently viewing DIAMOND AKIRI KUPATA UGUMU WA KUCHAGUA NGOMA ZITAKAZOPATIKANA KWENYE ALBUM MPYA

DIAMOND AKIRI KUPATA UGUMU WA KUCHAGUA NGOMA ZITAKAZOPATIKANA KWENYE ALBUM MPYA

Staa wa muziki wa Bongofleva Diamond Platnumz ameweka wazi kuwa album yake mpya itakuwa na jumla ya nyimbo 12 tu

Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa Instagram Diamond amesema mkononi ana jumla ya nyimbo 51 lakini anahitaji nyimbo 12 pekee kwa ajili ya albamu mpya ila anapata wakati ngumu kuchagua nyimbo atakazoziweka kwenye album yake.

Hitmaker huyo wa “Naanzaje” Diamond Platnumz amesema pia anafikiria kuachia EP kabla ya album ili kukata mashabiki kiu ya muziki kabla ya album hiyo.

Utakumbuka hadi sasa Diamond ametoa albamu kama Kwamwambie ya mwaka 2010, Lala Salama ya mwaka 2012 na A Boy From Tandale ya mwaka 2018.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke