Staa wa bongofleva Diamond Platnumz ameamua kuzitumia ipasavyo pesa anazozitolea jasho.
Mkali huyo wa Naanzaje ametumia kiasi cha dolla 25,000 ambazo ni zaidi ya shilling milioni 2.8 kwa pesa ya Kenya kununua saa mpya aina ya Rolex.
Hii ni kwa mujibu wa risiti ya ununuzi wa saa hiyo ambayo aliishare kwenye insta story yake kwenye mtandao wa Instagram.
Diamond Platnumz ambaye kwa sasa yupo nchini Marekani kwenye ziara yake ya kimuziki, alitembelea duka maarufu la Watch Empire huko Los Angeles na kujipatia saa hiyo yenye warantii ya miaka miwili.
Diamond anaungana na mastaa kama Davido, Drake, Jay Z, Kanye West ambao hupendelea kuvaa saa za aina ya Rolex.