Mwanamuziki wa Bongofleva Diamond Platnumz ametangaza kushirikiana na Rihanna kwenye Album yake ijayo.
Akizungumza na BBC akiwa huko nchini Uingereza Diamond Platnumz amesema kuwa tayari ameshaweka mambo sawa kukamilisha kolabo na staa huyo mkubwa wa muziki duniani na anaamini itakuwa ni moja kati ya nyimbo kubwa kuwahi kutokea.
“Napenda kufanya kazi na Rihanna, naona itakuwa nyimbo kali sana. Natumaini kama sio kwenye album yangu hii ijayo au nyingine tunaweza kushirikiana. Tumeshafanya mazungumzo toka mwaka jana kama sikosei. Anaweza kukosekana kwenye album hii kwasababu ya hali aliyonayo lakini kwa album inayofuata naamini tutakuwa pamoja”, amesema Diamond
Diamond kwa sasa yupo nchini Uingereza kwa ajili ya kui-promote EP yake mpya FOA ambayo ameiachia wiki chache zilizopita.