Msanii wa Bongofleva, Diamond Platnumz na baby mama wake, Zari The Bosslady ni miongoni mwa Mastaa wa Afrika watakaonekana katika mtandao wa Netfflix Machi 18, mwaka wa 2022.
Netflix tawi la Afrika Kusini limetangaza Mastaa hao wataonekana katika documentary waliyoipa jina la Young, Famous & African.
Ikumbukwe Diamond atakuwa Mtanzania mwingine kuonekana Netflix baada ya Idris Sultan ambaye Machi 26, mwaka 2021 alionekana kwenye mtandao huo kupitia filamu iitwayo ‘Slay’ iliyokutanisha Mastaa wa Afrika kama Ramsey Noah, Fabian Adeoye Lojede, na wengine wengi.