Mwanamuziki wa Bongofleva Diamond Platnumz ameweka wazi kwamba hatoshiriki kwenye tuzo za Tanzania zilizoandaliwa na Baraza La Sanaa nchini humo BASATA, akihoji kuwa kama wasimamizi wa tuzo hizo wameshindwa kumpatia Mirabaha ni vipi wataweza kumpatia tuzo.
Kwenye mahojiano na The Switch ya Wasafi FM Diamond Platnumz ameeleza kuwa tuzo pekee anazozitaka na kuzikubali ni tuzo za upande wa digital platforms kwa kuwa tuzo hizo hazisemi uwongo.
“Kimsingi Rais wetu Mh. Samia Suluhu ana nia njema sana ya kuwasaidia wasanii . Lakini kama kuna watu wamepewa nafasi huku chini kushughulikia mirabaha inabidi waangaliwe wasije kuitia Doa serikali na nia yao njema . Kwa mfano kama mrabaha tu huwezi kunipa je , tuzo utanipa ? “ Amesema Diamond Platnumz.
Mbali na hayo Diamond amedai kuwa hakuzisikia tuhuma zilizotolewa na Harmonize kuwa amekuwa na tabia ya kumshusha kila msanii anayefanya vizuri kwa kusema kwamba hilo halina ukweli wowote kwani kila msanii ana nafasi ya kupata mafanikio yake na yeye haamini katika kuwafanyia figisu vijana wenzake.
“Sikufuatilia kusikiliza, mimi kuna vitu huwa sitaki kufuatilia kusikiliza ila kama aliongea hivyo, unajua huwezi kumkataza mtu kuongea anachota kuongea, lakini WCB hatuna mkataba au system ya kumshusha mtu au kumnyonya mtu Amesema Diamond.
Hitmaker huyo wa ngoma ya Gidi ameendelea kwa kusema kuwa “Ikitokea mtu akinizungumzia vibaya zamani nilikuwa naumia sana ila sasa hivi nimekuwa napuuza, kwangu ni Baraka kwa sababu unaponizungumzia vibaya kwenye kitu ambacho sijakifanya unafanya Mwenyenzi Mungu anibariki zaidi, so sikutaka kufuatilia lakini mwisho wa siku kilichozungumzwa watu watajua ukweli upi na kwenye uongo watajua” .
“Halafu mimi kufikia kwenye hatua ya kutaka kumzulumu mtu, kumshusha mtu, ni kwamba huamini katika wewe, mimi naami katika mimi sana ndio maana unaoka katika hii EP kuna kolabo chache sana.