You are currently viewing DIAMOND PLATINUMZ AZUA GUMZO MTANDAONI KUPITIA VIDEO YA WIMBO WAKE WA GIDI

DIAMOND PLATINUMZ AZUA GUMZO MTANDAONI KUPITIA VIDEO YA WIMBO WAKE WA GIDI

Mwanamuziki kutoka nchini Tanzania Diamond Platnumz amekosolewa mitandaoni kwa kutumia bendera yenye utata katika video ya wimbo wake mpya wa Gidi.

Moja ya kipande cha video katika wimbo wa Gidi kina bendera mbili za kibaguzi wa rangi zinazoonyeshwa wakati  Diamond akicheza huku nyingine akiwa na muonkeano wa Cowboy.

Bendera hiyo ni ya kundi la Shirikisho la majimbo ya kusini ya Marekani ambayo yalipigania kudumisha utumwa wa watu weusi kati ya mwaka wa 1960 na 1961 na  inaonekana kama ishara ya mivutano ya ubaguzi wa rangi nchini Marekani.

Jambo hilo limezua gumzo mtandaoni ambapo watumiaji wengi kwenye mitandao ya kijamii hasa wafrika wameshambulia Diamond Platinumz kwa hatua ya kutumia bendera hiyo ya kibaguzi kwenye video ya wimbo wake Gidi kwa sababu ina tafsiri ya moja kwa moja kwamba ameungana na wazungu katika kuwapiga vita ndugu zake Weusi.

Hata hivyo wamemshauri msanii Diamond pamoja na uongozi wake kuhariri upya video hiyo na kutoa sehemu ambazo zina muonekano wa bendera hiyo kwani hili litakuwa jambo zuri tena la busara kwa msanii kama yeye ambaye analenga kupenya katika soko la muziki la Marekani.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke