Mwanamuziki nyota wa BongoFleva Diamond Platnumz ametangaza kuachia EP yake ya kwanza tangu aanze muziki.
Kupitia ukurasa wake wa instagram Diamond amesema kwamba EP hiyo ambayo hajaipa jina, itatoka March 4 mwaka huu.
Hata hivyo hitmaker huyo wa ngoma ya “Gidi” bado haijaweka wazi idadi ya nyimbo zitakazopatikana kwenye EP hiyo ila ni jambo la kusubiriwa.
Mwishoni mwa mwaka jana Diamond alisema albamu yake mpya ipo mbioni kutoka na itakuwa na nyimbo 12 ingawa atalazimika kuachia Extended Playlist (EP) kwanza kwa sababu tayari ana nyimbo 51 zilizokamika.
Ikumbukwe kuwa EP hiyo pia itaachiwa siku moja kabla ya Tamasha la mwanamuziki Harmonize , Afro East Carnival linalo tarajiwa kufanyika March 5, 2022