You are currently viewing DIAMOND PLATINUMZ KUWASAJILI WASANII WAPYA WCB

DIAMOND PLATINUMZ KUWASAJILI WASANII WAPYA WCB

Mwanamuziki wa Bongofleva kutoka Diamond Platnumz ameweka wazi kwamba Mwaka huu kuna wasanii wapya ambao watatambulishwa ndani ya record label yaWCB.

Katika mahojiano na kituo cha BBC Swahili nchini Uingereza Diamond amesema kwamba Mwaka huu kuna baadhi ya wasanii wataondoka katika lebo hiyo na kwenda kujiendeleza wenyewe.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Mtasubiri” amedai kwamba atakuwa nao bega kwa bega mara baada ya kutoka katika Lebo hiyo na akaongezea kusema kuwa wcb haiwezi kuwa na wasanii wale wale kila siku.

Tayari kauli yake hii inahusishwa na kitendo cha mwanamuziki Rayvanny siku chache zilizopita kufuta utambulisho wa kuwa mwanamuziki aliye chini ya usimamizi wa record label ya WcB katika ukurasa wake wa instagram.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke