You are currently viewing DIAMOND PLATNUMZ ADOKEZA KUMSAINI ASLAY WBC WASAFI

DIAMOND PLATNUMZ ADOKEZA KUMSAINI ASLAY WBC WASAFI

Moja kati ya vitu ambavyo Diamond Platnumz alivizungumza usiku wa kuamkia leo katika uzinduzi wa album mpya ya Barnaba “Love Sounds Different” ni kuhusiana na uwekezaji katika muziki hapa nchini unavyoyumba.

Diamond ameeleza kwa undani namna wawekezaji wanavyosita kuingia katika muziki kwa sababu wakiangalia lebo kama WCB wakati fulani hali wanayoipitia hasa wasanii wake wakitaka kondoka inakua ni mshikemshike kitu ambacho Diamond amekisisitiza mbele ya Basata.

Pia Diamond alimuongelea msanii aslayisihaka akisema kwamba ni mtu ambaye anamkubali na ana uwezo mkubwa sana na kama angekuwa chini ya usimamizi wake mwenyewe angefika mbali.

“Kila mtu humu ndani anamjua Aslay, ana uwezo mkubwa sana, siongei kwa sababu niko hapa lakini Aslay angekuwa mikononi mwangu, asingekuwa huyu mnayemsikia, angefika mbali zaidi, au angepata mwekezaji mwingine hata kama siyo mimi, angefika mbali sana.” ameeleza Diamond

Aidha, Aslay anatajwa kuwa ameshasaini na kampuni ya Sony Music na dili hilo lipo mbioni kutangazwa

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke