Kampuni ya Millennium Stars Entertainment inayoratibu tuzo za Bongo Music Awards imepokea barua kutoka uongozi wa kampuni ya Wasafi Limited uliopendekeza kuondolewa kwenye mchakato wa Tuzo za Bongo Music Awards kwa msanii Diamond Platnumz kutokana na kuwa na ratiba ngumu itakayomzuia kupata muda wa kutosha kushiriki katika mchakato wa Tuzo za Bongo Music Awards 2022.
Pamoja na mambo mengine uongozi wa Wasafi Limited wamepongeza na kushukuru kuona wapenzi wa muziki nchini Tanzania wamempendekeza kwa wingi msanii huyo.
Kwa maana hiyo kampuni hiyo itamuondoa msanii Diamond Platnumz kwenye category zote alizokuwa amependekezwa muda wowote kuanzia sasa.
Aidha, kampuni ya Millennium Stars Entertainment inaomba radhi kwa changamoto yoyote itakayojitokeza kwa mashabiki wa msanii Diamond Platnumz.