Msanii maarufu wa Bongofleva na mmiliki wa Lebo ya WCB Wasafi, Diamond Platnumz analipwa takriban millioni 12 za Kenya kwa show za kimataifa anazofanya.
Hayo ni kwa mujibu wa Meneja wa msanii huyo, Sallam SK akiongea kwenye mahojiano yake hivi karibuni ambapo amesema kwa show za Tanzania bei hiyo inapungua.
“Milioni 230 hiyo ni nje ya Tanzania, hapa ndugu zetu lazima tutashusha. Kimsingi imewekwa kiwango hicho, kwa hiyo haziwezi kuwa show nyingi kama mwanzo” alisema Sallam SK.
Katika hatua nyingine, Sallam SK amepuzilia mbali madai ya kwenda kuwa Meneja wa Harmonize na Konde Music kama ilivyodaiwa mtandaoni, amesema kufanya hivyo ni kujishusha kwa kuwa ameridhika na WCB Wasafi.
Hata hivyo amekanusha stori za kuwahi kutoka kimapenzi na Baby mama wa Diamond Platnumz, Tanasha Donna ,kwa kusema kuwa yeye na mrembo huyo walikuwa marafiki wa muda mrefu.