Msanii nyota wa Bongofleva Diamond Platnumz ameamua kutoa ya moyoni baada ya meneja wake Babu Tale kumshinikiza amuoe Zuchu kutokana na video aliyoichapisha kwenye ukurasa wake Instagram akibusiana na hitmaker huyo wa “Sukari”.
Kulingana na comment yake akimjibu Babu Tale, hawezi kumuoa msanii wake Zuchu kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakiamini.
“Sasa nitamuoaje wakati ni Msanii wangu Bosi, hilo busu hapo lisiwatishe viongozi, ni salamu tu za Kijerumani” amesema Diamond.
Utakumbuka wawili hao wamekuwa na ukaribu sana kiasi cha kuzawadiana zawadi jambo lililofanya baadhi ya watukuamini kuwa Diamond na Zuchu wapo katika mahusiano ya kimapenzi.