You are currently viewing DIAMOND PLATNUMZ ATAJWA KULIPWA KSH. MILLIONI 11 KUTUMBUIZA KWENYE HAFLA YA AZIMIO LA UMOJA

DIAMOND PLATNUMZ ATAJWA KULIPWA KSH. MILLIONI 11 KUTUMBUIZA KWENYE HAFLA YA AZIMIO LA UMOJA

Mitandao ya nchini imeripoti kwamba Diamond Platnumz alilipwa KSh Milioni 1.2 kutumbuiza kwa kila Dakika Moja katika uwanja wa Kasarani kwenye hafla ya mwisho ya kampeni za chama cha Azimio la Umoja wikendi iliyopita.

Diamond Platnumz anatajwa kulipwa kiasi cha KSh milioni 11.9 kutumbuiza kwenye hafla hiyo kwa dakika 10 tu.

Utakumbuka baada ya Diamond Platnumz kutumbuiza katika uwanja wa Kasarani katika hafla ya mwisho ya mkutano wa kisiasa wa Azimio Mchekeshaji Eric Omondi aliwatolea uvivu wasanii wa Muziki nchini kwa kusema kwamba wamelala.

Eric Omondi ambaye kwa muda mrefu amekuwa akipigana kwa udi na uvumba kutetea muziki wa Kenya, alisema kwamba hana ubaya na Diamond ila inasikitisha sana kwamba katika halfa ya kihistoria kama ile ya Kasarani, hakuna msanii hata mmoja wa Kenya aliyepata hiyo nafasi.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke