Mwanamuziki na mtayarishaji wa maudhui nchini Diana Bahati, amemkingia kifua mumewe Kevin Bahati, kwa madai ya kutotumia akaunti yake ya Instagram kwa muda mrefu.
Akimjibu shabiki yake aliyetaka kufahamu kiini cha ukimya wa hitmaker huyo wa ngoma Adhiambo diana b kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema ukimya wa bahati umetokana na msanii huyo kujikita zaidi kwenye masuala ya kifamilia kwani anatumia muda wake mwingi na watoto wake.
Hapo awali, Bahati, alikuwa akiwafahamisha mashabiki wake kuhusu matukio yanayotokea kwenye maisha yake, huku akichapisha maudhui mengi kwenye ukurasa wake ndani ya siku moja.
Kwa sasa, ukurasa wa Bahati hauna maudhui mapya tangu alipolia hadharani wiki mbili zilizopita kuhusu masaibu yake ya kisiasa, mara baada ya chama cha jubilee kumpokonya tiketiya kuwania ubunge wa mathare kwenye uchaguzi wa Agosti 9 mwaka huu.
Tangu wakati huo, mwanamuziki huyo hajachapishaa kitu chochote kipya kwenye mitandao yake ya kijamii akiwaacha mashabiki zake njia panda.